Home Simba SC SIMBA YAKWEA PIPA KUWAFUATA AL AHLY

SIMBA YAKWEA PIPA KUWAFUATA AL AHLY


 PATRICK Rweyemamu,  meneja wa Klabu ya Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Aprili 9, nchini Misri. 

Leo Aprili 6 kikosi cha Simba kimeanza safari kutoka ardhi ya Tanzania kuifuata Misri ambapo watapitia Dubai na kufanya mapumziko na kesho Aprili 7 wataunganisha safari kuibukia Misri.

Rweyemamu amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watakwenda kufanya vizuri kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

“Tunashukuru Mungu tumekuwa tukipata matokeo mazuri Kwenye mechi za kimataifa, kikubwa ambacho tunaamini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi katika mechi yetu ya mwisho.

“Wachezaji ambao tupo nao wapo tayari na wanahitaji kufanya vizuri tunaamini itakuwa hivyo, Watanzania na wadau watuombee ili tukafanya vizuri, ” amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo Kwenye msafara wa leo ni pamoja na Luis Miquissone,  Clatous Chama na Beno Kakolanya. 

SOMA NA HII  MGUNDA:- SIMBA WASAHAU KABISA.....