Home Habari za michezo MGUNDA ATAJWA ISHU YA DOGO WA SIMBA KUFUNGA JUZI…ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI…

MGUNDA ATAJWA ISHU YA DOGO WA SIMBA KUFUNGA JUZI…ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI…

Habari za Michezo

Straika mpya wa Simba, Mohammed Mussa aliyesajiliwa kupitia dirisha dogo lililofungwa Januari 15 mwaka huu, juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam amefunga bao lake la kwanza akiwa na kikosi hicho na kukiri akitabiriwa mapema na Kocha Juma Mgunda.

Mussa aliyekuwa Malindi ya Zanzibar na kuifungia mabao saba kabla ya kusajiliwa na Simba baada ya kung’ara katika michuano ya Mapinduzi 2023 alifunga bao la tatu la timu hiyo wakati wakiifumua Africans Sports kwa mabao 4-0 katika mechi ya 16 Bora ya michuano ya ASFC.

Mara baada ya kufunga bao hilo dakika ya 69, ikiwa ni muda mchache tangu atokee benchi kuchukua nafasi ya Habib Kyombo, mshambuliaji huyo alishangilia kwa kuvua jezi na kujikuta akilimwa kadi ya njano kwa kosa hilo. Mabao mengine ya Simba jioni hii yamewekwa kimiani na Jean Baleke, Kennedy Juma na Jimmyson Mwanuke.

Mara baada ya pambano hilo kumalizika na Simba kujihakikisha kufuzu robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho ikiwa timu ya kwanza, Mussa amefunguka akisema kabla ya mechi kocha Mgunda alimtabiria angefunga bao, ndio maana klipofunga alishangilia kwa furaha hadi kuvua jezi huku akimfuata kocha huyo kwenye benchi.

“Kocha aliniambia mapema kwamba leo nitafunga bao na kweli baada ya kuingia nilitumia nafasi niliyopata kuandika bao la tatu kwa timu na kunifariji mno. Nimefurahi kuifungia timu yangu bao na naamini nikiendelea kuaminiwa nifanya makubwa zaidi hapa,” amesema Mussa.

Kocha Mgunda alikiri juu ya kumtabiria Mussa na kumuelezea ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa akimtia moyo hasa baada ya kupoteza nafasi kadhaa kwenye mechi za nyuma alizopewa nafasi ya kucheza.

Simba iliyoanza juzi: Kakolanya, Mwenda, Gadiel, Kennedy, Ouattara, Mkude, Sakho, Nyoni, Kyombo, Phiri na Baleke

African Sports: Kaumbu, Gilla, Mwadua, Mwaluseke, Yona, Isidory, Michael, Kimenya, Bashir na Mtumbuka

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUISAIDIA YANGA KIPESA...ENG HERSI KAIBUKA NA JIBU HILI....KAMTAJA MANJI PIA...