Home Uncategorized YANGA: AGOSTI 30 TUNA JAMBO LETU, KONDE BOY NAYE NDANI

YANGA: AGOSTI 30 TUNA JAMBO LETU, KONDE BOY NAYE NDANI

 

HAMAD Seneda, maarufu kama Madee ambaye ni shabiki wa Yanga amesema kuwa haamini kama Agosti 30 kuna mtu atabaki nyumbani na kushindwa kutokea Uwanja wa Mkapa ambapo kutakuwa na jambo kubwa la kitaifa.


Madee ambaye yeye ni mwana Bongo Fleva amesema kuwa anaamini kuwa siku ya Agosti 30 ambayo ni kilele cha siku ya Wananchi ni sikukuu kubwa ya kila shabiki na mdau wa masuala ya mpira.


“Siamini kwamba kuna watu ambao watakuwa nyumbani Agosti 30 na kushindwa kujitokeza Uwanja wa Mkapa kushuhudia burudani ya nguvu kutoka kwa Wananchi bado sijaamini.


“Unajua siku hiyo majembe mapya na wachezaji wa kitaifa na kimataifa watatambulishwa hivyo siyo ya kukosa kabisa mtu wangu,” amesema.


Mbali na Madee pia msanii mwingine Chege Chigunda mtoto wa kiumeni naye atakuwepo huku balaa la shoo likishushwa pia na Harmonize maarufu kama Konde Boy.


Siku hiyo ni siku maalumu kwa Yanga kuwatambulisha wachezaji wapya ambao watatumika kwa msimu wa 2020/21 ambapo miongoni mwa nyota wa ndani ni pamoja na Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Wazir Junior na Abdalah Shaibu maarufu kama Ninja huku wa kimataifa akiwa ni Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Michael Sarpong.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA NAMUNGO FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA EL HILAL OBEID