Home Simba SC SIMBA YASEPA NA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

SIMBA YASEPA NA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR

 MABINGWA watetezi Simba leo Aprili 21, Uwanja wa Kaitaba wamesepa na pointi tatu bila ukuta wao kuruhusu bao la kufungwa mbele ya Kagera Sugar .


Mchezo huo ambao ni wa mzunguko wa pili, Simba ilikwenda vyumba vya kubadilishia nguo ubao ukisoma Kagera Sugar 0-2 Simba.

Kipindi cha pili timu zote mbili zilipambana kusaka bao huku Kagera Sugar wakipambana kupata ushindi ngoma ikawa ngumu.


Ni Luis Miquissone dakika ya 13 alipachika msumari wa kuongoza kisha Chris Mugalu alipachika msumari wa pili dakika ya 24.


Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru,  ubao ulisoma Simba 2-0 Kagera Sugar.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 55 ikiawa tofauti ya pointi mbili na watani wa jadi Yanga wenye pointi 57.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHUHUDIA 'AKIBABULIWA CHA UCHUNGU'...PABLO ASALIMU AMRI KWA NABI...ADAI WALIZIDIWA KILA KONA...