Home Simba SC WACHEZAJI WALICHANGANYA BENCHI LA UFUNDI SIMBA

WACHEZAJI WALICHANGANYA BENCHI LA UFUNDI SIMBA

 SELEMANI Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wanapata tabu kupanga kikosi cha kwanza kutokana na ubora wa wachezaji wote walionao kikosini.

Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wakipambana na watani zao wa jadi, Yanga ambao wapo nafasi ya kwanza na pointi zao 57 huku wao Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 55.

Akizungumza , Matola amesema kuwa kitu ambacho kinalichanganya benchi la ufundi la Simba ni katika kupanga kikosi cha kwanza.

“Tuna wachezaji wazuri ndani ya kikosi cha Simba jambo hilo linatufanya tuwe tunapata tabu kwenye kupanga kikosi cha kwanza, hii inatokana na wachezaji wetu wote kuwa bora.

“Kuanzia Chama, (Clatous) Jonas (Mkude), Luis, (Miqiussone) John(Bocco), Morrison (Bernard) hawa wote ni wachezaji wazuri sasa wakati wa kupanga kikosi cha kwanza huwa tunapata tabu na hili linatuchanganya.

“Ila yote haya ni muhimu kuweza kufanya vizuri kwa sababu ili uweze kupata matokeo mazuri ni lazima uwe na kikosi kizuri na chenye wachezaji bora, hicho ndicho kinachofanya tufanye vizuri,” amesema Matola.

Mechi mbili wakiwa nje ya Dar wameweza kukusanya pointi sita na mabao matatu huku ngome yao ya ulinzi ikiwa haijaruhusu bao.

Ilishinda kwa tabu mbele ya Mwadui FC hii ni kwa mujibu wa Matola, pale ubao uliposoma Mwadui 0-1 Simba na Kagera Sugar 0-2 Simba.

SOMA NA HII  SIMBA QUEENS WAKABIDHIWA NDINGA MPYA