Home Habari za michezo KUELEKEA DIRISHA DOGO….FADLU KATUMA MAOMBI HAYA KWA MABOSI SIMBA..

KUELEKEA DIRISHA DOGO….FADLU KATUMA MAOMBI HAYA KWA MABOSI SIMBA..

Habari za Simba- Fadlu Davids

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema anahitaji miezi minne kuendelea kuboresha kikosi chake kwani muda huo kitakuwa tishio kwa wapinzani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kimataifa.

Amesema anaimani wakati huu wanatafuta matokeo mazuri katika michezo ya ligi kuu, anaendelea kukinoa kikosi na kuirejesha Simba ya misimu ya nyuma inayopiga soka safi ‘pira biriani’.

“Ndani ya miezi hiyo tutakuwa tumeongeza wachezaji wapya kipindi cha dirisha dogo nitakuwa nimeshakiona kikosi changu, klabu yoyote inaposajili wachezaji zaidi ya 10 na kocha mpya inatakiwa kupata muda wa miezi sita kuona kiwango na muunganiko wa wachezaji,” amesema Fadlu.

Amesema kufahamu tabia za wachezaji, mikimbio, sifa, mifumo na udhaifu wa kila nyota kusaidiana uwanjani, walianza ligi na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika akiwa anajenga kikosi.

“Kwa sasa tunaendelea kumalizia ujenzi wa kikosi na mabadiliko yameonekana na kupiga hatua hadi Februari 2025, kikosi kitakuwa kimeshakamilisha kiufundi na kurejea katika ubora wa misimu ya nyuma,” amesema Kocha huyo.

SOMA NA HII  MERIDIAN WAIBUKIA KIJITONYAMA