Home Yanga SC YANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA BIASHARA UNITED

YANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA BIASHARA UNITED


 UONGOZI wa Yanga mapmbano yanaendelea na watasaka pointi tatu kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 17. Walipokutana Uwanja wa Karume, Mara Yanga ilisepa na pointi tatu baada ya Michael Sarpong kupachika bao la ushindi.

Kwenye msimamo wa ligi, Biashara United ipo nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 24 imekusanya pointi 40.

Inawafuata Yanga ambao ni vinara wakiwa na pointi 51 nao pia wamecheza jumla ya mechi 24.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:”Jumamosi ya mapambano ya alama tatu inakuja hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti.

“Ipo wazi kwamba tunaongoza ligi na wachezaji wana morali kubwa wakati mwingine matokeo ya mpira yamekuwa tofauti ila ni mpira,” .

SOMA NA HII  MAYELE AONYESHA 'MAHABA' YA WAZI KWA MASTAA WA SIMBA...AWAITA KWENYE KIKOSI CHAKE BORA CHA MSIMU...