KOCHA Mkuu wa kikosi cha Liverpool, Jurgen Kloop amesema kuwa maisha ni mafupi hivyo hawezi kuwa na hofu juu ya mafanikio ya timu zote za Manchester na anamini kwamba msimu ujao atakuwa imara na ushindani utakuwa mkubwa kwake.
Pep Guardiola upande wake amekuwa akipewa nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu England na anapewa nafasi ya kuipeleka timu yake ya Manchester City hatua ya fainali ya Champions League kwa kuwa nusu fainali ya kwanza alishinda mbele ya Paris Saint Germain, (PSG).
Wakati huo Manchester United wao kwenye Europa League nusu fainali ya kwanza walishinda mabao 6-2 dhidi ya Roma.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England, Liverpool wamekuwa katika wakati mgumu kuweza kutwaa taji hilo huku wakiwa hawana uhakika wa kumaliza ndani ya nne bora.
“Hiyo kwangu sio tatizo, tatizo langu kubwa ni kwa wale wapinzani wangu ambao nitakutana nao wikeendi hii na sio kufikiria habari nyingine, Oh Mungu wangu, City tena na United kurejea kwenye ubora wao.
“Maisha ni mafupi sana kwa haya ambayo yanatokea hii ni aina ya tabia ambayo haina haja ya kuwa na hofu nayo. Tutapata changamoto kubwa msimu ujao lakini kwa mwaka huu bado tunaangalia ni namna gani tutamaliza msimu huu hatuna cha kufanya kwa wale ambao wapo nusu fainali na nusu fainali,” amesema.