Home Yanga SC YANGA WATUA SALAMA DAR

YANGA WATUA SALAMA DAR

 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nassreddine Nabi kimewasili salama leo Mei Mosi Dar es Salaam,  kikitokea Mbeya.


Jana Aprili, 30 Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Tanzania Prisons hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho. 


Timu hiyo ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Yacouba Songne raia wa Burkina Faso dakika ya 53.


Kwa ushindi huo Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na inasubiri droo kuchezwa hivi karibuni ili kujua wapinzani wao.


Miongoni mwa timu ambazo zimetinga hatua  ya robo fainali ni pamoja na Mwadui FC,  Rhino Rangers na Azam FC. 


Leo Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Kagera Sugar,  Uwanja wa Mkapa, Dodoma FC v KMC.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPIGWA NA WAARABU WEUSI...CAF WAIPA YANGA WAARABU WEUPE....WAKISHINDWA NA HAPO WATABAKI 'KUCHAMBUA MCHELE'...