Home Yanga SC ORODHA YA NYOTA SITA YANGA AMBAO MIKATABA YAO INAELEZWA KUFIKA UKINGONI

ORODHA YA NYOTA SITA YANGA AMBAO MIKATABA YAO INAELEZWA KUFIKA UKINGONI


IMEELEZWA kuwa miongoni mwa nyota wa kikosi cha Yanga kwa sasa wanacheza wakiwa wanatambua kwamba mikataba yao inakaribika kufika ukingo msimu utakapomeguka 2020/21.

Miongoni mwa nyata hao ni pamoja na mshambuliaji Fiston Abdulazack ambaye amefunga mabao mawili kwa timu hiyo, moja ilikuwa ni kwenye ligi na moja kwenye Kombe la Shirikisho.

Deus Kaseke winga huyu mzawa amekuwa kwenye ubora wake ambapo kibindoni ametupia mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara.

Juma Makapu beki huyu mzawa ameanza kupewa nafasi kikosi cha kwanza taratibu kwa sasa.

Saido Ntibanzokiza kiungo huyu mshambuliaji amekuwa ni mwenye hasira akianzia benchi na amefunga mabao matatu ndani ya ligi.

Metacha Mnata huyu ni kipa namba moja wa Yanga ambapo inaelezwa kuwa tayari mabosi wake wameanza kufanya naye mazungumzo.

Paul Godfrey beki huyu wa pembeni hana nafasi kikosi cha kwanza msimu huu.


SOMA NA HII  CARLINHOS AKABIDHIWA MAJUKUMU YA SAIDO YANGA