epl

SALAH HAJUI LOLOTE KUHUSU MKATABA WAKE NDANI YA LIVERPOOL

admin May 2, 2021 9:47 am


 MOHAMED Salah, mshambuliaji wa Liverpool amesema kuwa hakuna ambaye amemfuata kwa sasa kuzungumza naye kuhusu suala la kuongeza mkataba wake.

Mkataba wa awali wa Salah ndani ya Liverpool unatarajiwa kumeguka Juni 2023 na inaonekana kwamba hakuna mpango wa nyota huyo kuongezewa mkataba.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Barcelona pamoja na Real Madrid tangu msimu uliopita.

Raia huyo wa Misri amesema kuwa hakuna ambaye amemfuata kuzungumza naye kuhusu suala la mkataba wake jambo ambalo hawezi kulizungumzia kwa sasa.

“Hakuna ambaye anazungumza na mimi kuhusu mkataba hivyo siwezi kusema zaidi. Ndani ya klabu hakuna ambaye anazungumza na mimi kuhusu mkataba hivyo kwa sasa sijui lolote na siwezi kuzungumza.

“Tusubiri na tuone, muda utazungumza kwa kuwa mimi sijui lolote lile,” .

Salah alitua kikosini hapo 2017 amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya na akiwa ni mfungaji bora mara mbili. 

Leo kikosi chake kinachonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp, kina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Manchester United mchezo wa Ligi Kuu England.

UMAFIA, SIMBA WAICHAMBUA YANGA KWA MTINDO HUU, WATAJA MAKOSA YAO SIKU 100  TAMU ZA GOMES AKIWA NA SIMBA SC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply