UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa unaamini utafanya vizuri kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho na kufikia malengo ya kutwaa taji hilo lililo mikononi mwa Simba.
Azam FC imetinga hatua hiyo ya robo fainali baada ya kupata ushindi mbele ya Polisi Tanzania ambapo ilishinda mabao 2-0, Uwanja wa Azam Complex.
Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa wanaimani na mipango iliyopo jambo linalowapa nguvu ya kuweza kufanya vizuri.
“Tupo imara na mipango ipo kamili, kikubwa ni kuona kwamba mechi zetu zijazo tunashinda na kupata matokeo chanya, mashabiki wazidi kutupa sapoti.
“Bado kazi inaendelea kwani wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kufikia malengo ambayo tumeweka na hilo lipo wazi kwani bado jambo letu linaendelea,” amesema.
Azam FC inanolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina aliwahi kuifundisha timu ya Yanga ambapo ubao ulisoma Yanga -1 Azam FC.