Yanga SC

YANGA: HATUNA HOFU NA SIMBA

admin May 7, 2021 9:47 am


NASSREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anatambua kwamba timu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ni timu nzuri ila hana hofu kuelekea mchezo wa kesho Uwanja wa Mkapa.

Nabi kesho atakutana na Gomes wa Simba katika mchezo wa Kariakoo Dabi utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 hivyo kesho utakuwa ni mchezo wa kukata na shoka kwa timu zote mbili kuwania pointi tatu.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 57 na Simba ipo nafasi ya kwanza imekusanya pointi 61.

Nabi amesema:”Ninaitambua Simba, nimewahi kukutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa hata kocha wao Gomes, (Didier) ninamtambua.

“Licha ya kwamba Simba ni timu kubwa sina hofu nao nina amini kwamba kila timu ina mbinu zake na aina ya kufanya katika kutafuta matokeo,” amesema. 

VIDEO: SHABIKI ALIYEJICHORA NEMBO YA SIMBA ATAJA SABABU YA KUIPENDA TIMU HIYO CARLINHOS AWAHISHWA HOSPITALI FASTA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply