MCHAMBUZI wa masuala ya michezo na beki wa zamani wa kikosi cha Manchester United, Gary Nevile amesema kuwa kuongeza mkataba mpya kwa nyota Edinson Cavani kutasimamisha mpango wa timu hiyo kumsajili Harry Kane ama Erling Haaland.
Ilikuwa inaelezwa kuwa Manchester United ina mpango wa kumsajili Kane mshambuliaji wa Tottenham Hotspur pamoja na Haaland mshambuliaji wa Borussia Dortmund ambao walikuwa wanahusishwa kuwa ndani ya Old Trafford msimu ujao.
United walikuwa wanapambana na Chelsea, Manchester City, Real Madrid na Barcelona kumpata Haaland ambapo dau lake lilikuwa linatajwa kuwa ni pauni milioni 154 ila kitendo cha kumuongezea Cavan dili la mwaka mmoja kutawafanya wapunguze kasi ya kuwania saini za nyota hao.
Nevile anaamini kwamba kwa sasa United hawahitaji kuongeza mshambuliaji mwingine kwa sababu Cavan amekuwa mwenye ubora kwa sasa ndani ya Uwanja katika kutimiza majukumu yake.
“Kwa namna ambavyo ninaona sera ya Ole tangu awasili ndani ya United amekuja kwa namna anavyokwenda sidhani kama wanaweza kuongeza mshambuliaji mwingine. Labda itatokea ila ukumbuke kwamba kuna wachezaji wengine waliachwa msimu uliopita licha ya kwamba walikuwa wanahusishwa kusajiliwa na timu hiyo,” .