Home Simba SC GOMES ATAJA WACHEZAJI WAWILI ATAKAOWAONGEZA SIMBA SC

GOMES ATAJA WACHEZAJI WAWILI ATAKAOWAONGEZA SIMBA SC


KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesisitiza kwamba hafikirii kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake, lakini akataja nafasi mbili atakazonunua mastaa wapya ili kuzidi kukinukisha.

Tayari juzi Gomes alishaweka wazi kwamba wachezaji 17 wazawa hatawapiga chini hata mmoja labda waamue wenyewe kuondoka kwa sababu zao binafsi.

Akizungumza Soka la Bongo Gomes safari hii ametamka kwamba anafikiria kufanya usajili makini sana kwenye nafasi mbili muhimu ndani ya kikosi hicho, ile ya ulinzi na ushambuliaji.

“Katika kikosi changu kama maboresho yanaweza kutokea basi binafsi mtazamo wangu ni maeneo mawili, beki wa kati pamoja na kiungo mshambuliaji,” alisema Gomes ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kwa sasa.

“Simba ni moja ya kikosi chenye wachezaji bora katika mashindano ya ndani pamoja na kimataifa ambayo nina imani kubwa msimu ujao tutafanya vizuri zaidi ya msimu huu,” aliongeza Gomes ambaye leo anakiwasha na Namungo ugenini katika VPL.

Kocha huyo anaamini kwamba sura hizo mbili zikiongezeka kwenye kikosi chake atafanya vizuri zaidi na timu itakuwa na machaguo mengi imara.

Alisema kwamba anafikiria kununua wachezaji hao kutoka popote pale lakini bado hajapata machaguo ya mwisho kwavile anapambania kwanza ubingwa kuhakikisha Simba inautetea na kubeba pia lile la Shirikisho (ASFC).

Wachezaji kumi wa kigeni waliopo Simba sasa wanaocheza na ligi ya ndani ni Joash Onyango, Pascal Wawa, Taddeo Lwanga, Luis Miquissone, Clatous Chama, Larry Bwalya, Bernard Morrison, Chriss Mugalu, Meddie Kagere na Parfect Chikwende.

Francis Kahata ambaye kwa duru za ndani zinavyoeleza, ana nafasi kubwa ya kubaki Simba yeye anacheza mashindano ya kimataifa tu na mkataba wake siku zinahesabika.

Kuhusu usajili wa wazawa alisema hatarajii kumtema yoeote kwavile anaona hao alionao wana uwezo mkubwa kuliko wengine anaowaona kwa washindani wake.

SOMA NA HII  BAADA YA MASHABIKI KUANZA KUMNANGA...MGUNDA AIBUKA NA KUANIKA MSIMAMO WAKE NA SIMBA...