Home Azam FC AZAM KUANZA MAZOEZI KESHO

AZAM KUANZA MAZOEZI KESHO

[the_ad id="25893"]

 


BAADA ya kumaliza siku nne za mapumziko, kikosi cha klabu ya soka ya Azam kesho kinatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina.

Baada ya mchezo huo wa robo fainali ya kombe la FA uliopigwa Mei 26, mwaka huu dhidi ya Rhino Rangers, Uongozi wa Azam uliwapa mapumziko ya siku nne wachezaji wote, ambayo yanamalizuika leo Jumapili, na kesho wataanza rasmi mazoezi ya kujiwinda na mchezo dhidi ya Gwambina.

Akizungumzia mipango yao, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kikosi chetu kinatarajia kuanza rasmi mzoezi kesho, Jumatatu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Gwambina ambao utachezwa Juni 18, mwaka huu.

SOMA NA HII  AZAM FC BADO INAUFIKIRIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here