Home epl HAKUNA MCHEZAJI KAMA KANTE

HAKUNA MCHEZAJI KAMA KANTE

[the_ad id="25893"]


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Martin Samuel amesema kuwa hakuna mchezaji kama kiungo mkabaji, N’Golo Kante ambaye anacheza ndani ya kikosi cha Chelsea kinachonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel kutokana na jitihada zake binafsi kwenye kutimiza majukumu yake.


Kante ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni ametwaa mataji sita huku akiwa katika ubora wake uleule. Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Manchester City aliweza kukata umeme kwa asilimia 100 bila kusababisha hata faulo moja.

Samuel amesema kuwa Kante ana nafasi ya kuweza kuingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka 2021 bila mashaka pamoja na Robert Lewandowski ambaye amefunga jumla ya mabao 20 katika mechi 48 msimu huu akiwa ndani ya Bayern Munich.

Kante ameshinda Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Ufaransa, ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameshinda taji la Europa na ana mataji mawili ya Ligi Kuu England pamoja na taji moja la FA akiwa chini ya makocha watano tofauti.

Samuel amesema:”Unaweza kuona namna gani anafanya na kwa uwezo wake kwa sasa hakuna ambye anafanya kama yeye hasa kwa namna ambavyo anajali wengine kuliko yeye binafsi, wapo wengi ambao walikuwa bora ila yeye anaonyesha uimara wake katika mapambano,” .

SOMA NA HII  ROBERT LEWANDOWSKI MWAMBA ANAYETABASAMU HUKU AKIWALIZA WENGINE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here