Home news KOCHA MPYA BIASHARA UNITED AANZA KAZI

KOCHA MPYA BIASHARA UNITED AANZA KAZI


PATRICK Odhiambo Okumu, raia wa Kenya ambaye amepewa mikoba ya Francis Baraza kuinoa Klabu ya Biashara United amesema kuwa yupo tayari kuifundisha timu hiyo yenye maskani yake Mara.

Baada ya kutambulishwa tayari jana, Mei 5 alianza kukinoa kikosi hicho ambacho kinajiandaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji.

Okumu ambaye ni maarufu kwa jina la Patto amewahi kufundisha Gor Mahia FC, Kakamega FC pamoja na Kakamega FC ambapo kote huko alikuwa ni Kocha Msaidizi.

Mei 4 alitambulishwa rasmi na uongozi wa Biashara United iliyo nafasi ya 4 na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 28.

Kocha huyo amesema:”Nipo tayari kwa ajili ya kufanya kazi na Biashara United, naamini kwamba ushindani ni mkubwa ila hakuna mashaka kwa kuwa ni muhimu kuwa na ushirikiano katika utendaji wetu,”.

SOMA NA HII  BAADA YA UKIMYA MWINGI ONYANGO AFUNGUKA HAYA