Home Yanga SC KUMBE INJINIA HUVAA JEZI YA KAIZER CHIEFS AKIWA NA FURAHA

KUMBE INJINIA HUVAA JEZI YA KAIZER CHIEFS AKIWA NA FURAHA


MJUMBE wa Kamati ya Klabu ya Yanga katika masuala ya usajili, Injinia Hersi Said amesema kuwa huwa anavaa jezi ya Kaizer Chiefs pale anapokuwa na furaha.

Injinia ameongeza kuwa hiyo ilikuwa ni zawadi aliyopewa na mtoto wa mmiliki wa timu hiyo ya Afrika Kusini.

“Hii jezi ya Kaizer Chiefs nilipewa na mtoto wa mwenye timu katika siku ya maadhimisho ya timu hiyo ina historia nzuri kwangu ni ya miaka mingi imepita na hii jezi naivaa siku ambayo nikiwa na furaha,”.

Jana Mei 19 wakati ubao wa Jamhuri, Dodoma ukisoma JKT Tanzania 0-2 Yanga injinia aliutinga uzi huo ikiwa ni ishara ya furaha kwake.

Pia kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe mrefu kuelezea jezi hiyo ambapo alisema kuwa alipewa uzi huo mwaka 2020.

Jina la mtoto wa mmiliki wa timu hiyo ambayo alitoa mualiko kwa Yanga ulisimamiwa na Bobby Kaizer ambaye ni Meneja wa timu hiyo.

Ilikuwa ni katika sherehe ya kuazimisha miaka 50 ya timu hiyo ambapo na wao waliwakabidhi Kaizer Chiefs jezi ya Yanga yenye chapa ya GSM.


SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUMTEMA MKUDE KOCHA WA YANGA KUAMUA JAMBO HILI