Home Uncategorized SIMBA: YANGA ITAKUTANA NA BALAA LA BWALYA

SIMBA: YANGA ITAKUTANA NA BALAA LA BWALYA

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambayo inatarajiwa kupigwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa imepangwa mapema sana jambo ambalo linawapa hasira ya kujipanga vizuri.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa alipoona ratiba alishangaa kwa kuwa wao wameshakiweka kikosi tayari na wapo tayari kwa ushindani huku akisisitiza kuwa wapinzani wao hao watakutana na balaa la nyota kama Larry Bwalya na Luis Miquissone.

 

“Wale wenzetu tunakutana nao Oktoba 18 mwaka huu kwenye ligi, dah! Itakuwa balaa, mbona wametufanya tukutane mapema, yaani sijui itakuwaje, maana hilo mbungi litakalopigwa siyo la nchi hii.

 

“Fikiria una mtu kama Bwalya (Larry), Miquissone (Luis), Chama (Clatous) hapo ujue wengine sijawataja mimi sijui itakuwaje, ila tusubiri na tuone,” alisema Manara.


Bwalya ni ingizo jipya ndani ya Klabu ya Simba alitambulishwa rasmi siku ya kilele cha Simba, Agosti 22, wakati wakicheza dhidi ya Vital’O ya Burundi ambapo Simba ilishinda mabao 6-0 huku yeye akitoa pasi moja ya bao Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  AZAM FC WATAKA KUCHEZA MECHI MBILI TU KAGAME