Home Yanga SC YANGA YATUMA SALAMU KWA WATANI ZAO SIMBA

YANGA YATUMA SALAMU KWA WATANI ZAO SIMBA


 UONGOZI wa Yanga umetamba kuwa kikosi 
chao kimejipanga vizuri kuhakikisha kinaibuka na pointi tatu katika kila mchezo ulio mbele yao, ukiwemo mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Julai 3, mwaka huu.

Yanga iliyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 61 baada ya kucheza michezo 29, wataivaa Simba katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza klabu hizo zilitoa sare ya bao 1-1, Novemba 7, mwaka jana.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema:-“Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi alitoa muongozo wa kuendelea kwa programu za mazoezi, licha ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wetu walio kwenye majukumu ya timu za taifa.

“Hii ni katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na utayari wa kufanya vizuri katika michezo yetu mitano ijayo ikiwemo mchezo dhidi ya Simba, kwetu michezo hiyo yote ina hesabu za pointi tatu katika kila mchezo bila kuangalia ukubwa au udogo wa wapinzani tutakaokutana nao.”

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ni namba moja wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wapo timu ya taifa inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi, Juni 13 ni pamoja na Feisal Salum, Dickson Job, Metacha Mnata na Bakari Mwamnyeto.


SOMA NA HII  GAMONDI AWAPOTEZEA SIMBA, ASEMA HAYA KUHUSU YANGA KUKUTANA NA SIMBA