Home Azam FC AZAM FC KAMILI KWA AJILI YA NAMUNGO FC

AZAM FC KAMILI KWA AJILI YA NAMUNGO FC


UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Namungo FC utakaochezwa kesho, Uwanja wa Majaliwa.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 63 baada ya kucheza jumla ya mechi 31.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 2-2 Namungo hivyo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zote zijazo hivyo watapambana kupata pointi tatu. 

Ikumbukwe kwamba Azam FC imetoka kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Gwambina FC kwenye mchezowa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mpiana Monzizi na Idd Seleman nyota hawa walitupia mabao mawilimawili kila mmoja.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA AZAM FC KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA, KOMBE LA SHIRIKISHO