epl

SANCHES AINGIA ANGA ZA ARSENAL

admin June 27, 2021 10:47 am


KIUNGO wa timu ya taifa ya Ureno anayekipiga ndani ya Klabu ya Lille inayoshiriki Ligue 1, Renato Sanches amewekwa kwenye rada za Arsenal na Liverpool za England. 

Nyota huyo mwenye miaka 23, leo Juni 27 anatarajiwa kuwa katika kikosi kitakachopambana na Ubelgiji katika hatua ya 16 bora Euro 2020.

Ripoti zinaeleza kwamba, Kocha Mkuu wa Arsenal,  Mikel Arteta anamfuatilia kwa ukaribu nyota huyo ili ajiunge nao msimu ujao katika eneo la kiungo.

Kwenye Euro 2020 alianza mchezo mmoja kikosi cha kwanza huku michezo miwili akitokea benchi na aliweza kuonyesha kiwango bora kwa timu hiyo jambo ambalo limezivutia timu nyingi.


HII HAPA MITIHANI MINNE  ILIYOSALIA YA GOMES NDANI YA SIMBA MANJI NDANI YA MKUTANO WA YANGA LEO JUNI 27

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply