Home Simba SC CHIKWENDE PERFECT AWAGAWA SIMBA ISHU YA KUVUNJIWA MKATABA

CHIKWENDE PERFECT AWAGAWA SIMBA ISHU YA KUVUNJIWA MKATABA

 IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Perfect Chikwende amewagawa viongozi wa Simba kutokana na wengine kuvutana wakitaka abaki na wengine wakihitaji avunjiwe mkataba wake.

Nyota huyo alisajiliwa katika usajili wa dirisha dogo akitokea Klabu ya FC Platinum inayoshiriki Ligi Kuu ya Zimbabwe.

Jina lake lilimuengua Francis Kahata kucheza Ligi Kuu Bara na kupelekwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na baada ya Simba kutolewa hatua ya robo fainali Kahata hakuongezewa dili jipya.

Habari zinaeleza kuwa wapo ambao wanahitaji asepe kwa kuvunja mkataba ila wanahofia gharama za kusitisha mkataba huo na wengine wanataka abaki.

“Mabosi wanafikiria abaki ama aondoke ila katika kuvunja mkataba ni gharama. Inawezekana akaachwa na akasajiliwa mshambuliaji mwingine, hivyo ni suala ambalo limeleta mgawanyiko, ” ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah, alisema kuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes ndiye mwenye maamuzi kuhusu wachezaji watakaobaki na kusajiliwa.


SOMA NA HII  KWA SOKA LA SIMBA YA MBRAZILI...IPO SIKU KUNA TIMU ITAKULA 20... HUYO NTIBAZONKIZA KAMA MPYAA...