Home Azam FC DUBE AIWEKA KANDO TUZO YA MEDDIE KAGERE

DUBE AIWEKA KANDO TUZO YA MEDDIE KAGERE


 KINARA wa mabao ndani ya ardhi ya Bongo katika Ligi Kuu Bara, Prince Dube amesema kuwa hana mpango wa kufikiria kutwaa tuzo ya kiatu bora kwa sasa zaidi ya kufikiria matokeo chanya kwa ajili ya timu hiyo.

Dube ametupia jumla ya mabao 14 anafuatiwa na mzawa, John Bocco mwenye mabao 13 akiwa ndani ya Simba na ni namba moja kwa wazawa wenye mabao mengi.

Mwenye kiatu chake kwa msimu uliopita Meddie Kagere yeye ametupia mabao 11 ambapo anapambana kuona namna gani anaweza kufikia malengo yake.

Chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina, Dube amekuwa ni chaguo la kwanza jambo ambalo linampa nafasi ya kufunga mabao mengi zaidi kwa msimu huu wa 2020/21 ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC.

Nyota huyo amesema:”Furaha kubwa kwangu ni kuona kwamba timu inashinda masuala ya kufikiria kuwa na tuzo kwa sasa hapana, ila kikubwa ni kuona kwamba tunafikia malengo ambayo tumejiwekea.

“Ikiwa timu itashinda basi hapo ni furaha kwangu na nikifunga ama kutengeneza nafasi ya bao ni sawa jambo la msingi ni kuona tunashinda mechi zetu,” amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 60 baada ya kucheza mechi 30 vinara ni Simba wenye pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.

SOMA NA HII  PAMOJA NA UWEPO WA MASTAA WAKUBWA ....DUBE APITISHWA AZAM FC...KOCHA MSOMALI AMPA MBELEKO ....