Home Simba SC DUH! SIMBA WAPIGWA MKWARA, WAAMBIWA HAWANA FEDHA KUMPATA BWALYA

DUH! SIMBA WAPIGWA MKWARA, WAAMBIWA HAWANA FEDHA KUMPATA BWALYA


SIMBA wameambiwa kwamba hawana hela ya kumlipa nyota wa kikosi cha Al Ahly, Walter Bwalya ambaye anatajwa kuibukia ndani ya kikosi hicho.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes imepanga kufanya maboresho kwenye upande wa safu ya ushambuliaji huku jina la Bwalya ambaye ni mali ya Al Ahly likitajwa.

Mshambuliaji huyo alikuwa akitajwa kuwaniwa na Simba kwa muda mrefu tangu akikipiga ndani ya Nkana FC  ya Zambia ila ikawa ngumu kwa mabosi hao kumpata akaaibukia El Gouna.

Akiwa ndani ya Al Ahyl ya Misiri ameshindwa kuonyesha makeke ndani ya kikosi hicho jambo ambalo linawafanya mabosi wafikirie kumuuza.

 Kwa mujibu wa wakala wa nyota huyo, Paricha Chikoye amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo mabosi wake wanataka kumuuza ila kuibukia ndani ya Simba itakuwa ngumu kutokana na mkwanja.

“Ipo wazi kwamba Al Ahly wanataka kumuuza mteja wangu kutokana na kuona kwamba haendani na mfumo ya timu yao hivyo hamna namna lazima wamuuze.

“Imekuwa tetesi kwamba anahitajika na Simba ila ukweli ni kwamba Simba hawana uwezo wa kumlipa fedha ambazo tunahitaji kutokana na mkataba wa kule Al Ahly.

“Kumpata Bwalya sio jambo jepesi na sisi tunahitaji fedha kubwa na siwezi kukutajia kwa sasa hivyo tusibiri na tuone,” amesema.


SOMA NA HII  BAADA YA CHAMA KUKOSA TUZO LA CAF....MDAU AIBUKA NA HILI KUKANDIA MFUMO WA KUPIGA KURA...