Home Tetesi za usajili HUYU HAPA KIUNGO MKABAJI WA KAIZER CHIEFS ANAYEPIGIWA HESABU NA YANGA

HUYU HAPA KIUNGO MKABAJI WA KAIZER CHIEFS ANAYEPIGIWA HESABU NA YANGA


 IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumsajili kiungo mkabaji anayecheza ndani ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini.

Nyota ambaye anapigiwa hesabu na Yanga anaitwa Anthony Akumu, ambaye ameletwa duniani Oktoba 20,1992 ana umri wa miaka 28 ni mzaliwa wa Rachuonyo, Kenya.

Ikiwa dili lake litakamilika kwa sasa ambapo mpanga mipango ni Injinia, Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ndani ya Yanga kutia timu Afrika Kusini.

Kiungo huyo miongoni mwa timu ambazo amecheza ni pamoja na Gor Mahia mwaka 2010-14, 2014-15, alikuwa ndani ya Al Khartoum, 2016-20 aliitumikia Zesco United na sasa yupo Kaizer Chiefs.

Pia katika timu yake ya taifa ya Kenya, kiungo huyo amecheza jumla ya mechi 38.

SOMA NA HII  SIRI ZA AZIZI KI ZAANIKWA WAZI....MAMA YAKE AFUNGUKA A-Z JINSI SIMBA WALIVYOMPAPATIKIA...