Home Yanga SC ISHU YA METACHA MNATA KUIBUKIA SIMBA, AZAM MPANGO UPO HIVI

ISHU YA METACHA MNATA KUIBUKIA SIMBA, AZAM MPANGO UPO HIVI

 

METACHA Mnata, anaweza kwenda Azam FC ama Simba ikiwa mabosi wake wa sasa Yanga watakaa kimya juu ya mkataba wake.

Nyota huyo ambaye amesimamishwa na Yanga kwa muda usiojulikana huku akikutana na rungu kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kutocheza mechi tatu pamoja na faini ya laki tano dili lake linameguka msimu huu.

Kosa lake ilikuwa ni kuwaonyesha ishara ya matusi mashabiki wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting,  Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 3-2.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mnata, Jemedari Said amesema kuwa yupo tayari kupokea ofa kutoka Azam FC na Simba endapo Klabu ya Yanga itakaa kimya.

“Kuhusu Metacha tunawasubiri Yanga wenyewe tuone ni jinsi gani tutaingia nao makubaliano mapya ya kimkataba, kama watashindwa basi sisi tupo tayari kusikiliza ofa ya timu yoyote,”.


SOMA NA HII  KAZE :- YANGA SC BILA YA NTIBAZONKIZA NA YACOUBA WASAHAU UBINGWA VPL