Home Simba SC KUHUSU WANAOSAJILI KUJA KUCHEZA NAMBA YAKE..ZIMBWE JR AMEFUNGUKA HAYA

KUHUSU WANAOSAJILI KUJA KUCHEZA NAMBA YAKE..ZIMBWE JR AMEFUNGUKA HAYA


SIMBA kwa misimu mitatu tofauti imekuwa ikisajili beki wa kushoto wa kumpa ushindani beki wao wa sasa aliyejimilikisha namba kikosi cha kwanza, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kwa sasa anatafutwa beki mwingine, lakini mwenyewe amesema wala hana presha yeyote.

Tshabalala, amesema kuwa, wachezaji hao ambao wamekuwa wakisajiliwa katika nafasi hiyo wamekuwa ni chachu zaidi ya kukua kwa kiwango chake kwani kadri apatavyo ushindani ndivyo anavyozidi kujibidiisha ili awe imara zaidi kuepuka kupoteza namba.

Alisema huwa anafurahia kupata changamoto na ushindani kwa vile humfanya asibweteke kama ambavyo angekuwa mwenyewe katika nafasi hiyo na kubwa kwake ni kutaka kuendelea kubaki kikosi cha kwanza.

“Kama unakumbuka katika mechi ya mwisho msimu uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar tulipochukua taji nilieleza msimu huu tunatetea tena ubingwa na tunakwenda kulitimiza hilo, hivyo kiu hii ya kutaka kuona inapata matokeo mazuri ndio inayonifanya nijitume zaidi mazoezi na uwanjani,” alisema Tshabalala.

Kwa misimu mitatu Simba imesajili mabeki wa kushoto akiwamo Asante Kwasi, Jamal Mwambeleko na Gadiel Michael ambao wote wameshindwa kufua dafu mbele yake Tshabalala na kwa sasa inaeleza mabosi wa klabu hiyo wanaendelea kusaka mwingine wa kuwaongeza nguvu.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- TUTAMUUNGA MKONO INONGA ILA SIO KUPAKA MKOROGO NA KUJA NAO UWANJANI..