Home Simba SC KUMBE! MORRISON ALIZUIWA KUSHANGILIA NA WACHEZAJI PAMOJA NA KOCHA

KUMBE! MORRISON ALIZUIWA KUSHANGILIA NA WACHEZAJI PAMOJA NA KOCHA


NYOTA wa kikosi cha Simba, Bernard Morrison amesema kuwa alipanga kushangilia kwa mtindo mwingine kabisa ila alizuiwa na wachezaji wenzake pamoja na kocha.

Walipocheza na Namungo, Morrison alifunga bao bora kwake ambalo mashabiki wa Simba ikiwa ni pamoja na Aggy Simba alisema kuwa lile ni bao bora la msimu kwa kuwa alilipachika akiwa nje ya 18.

Baada ya kufunga bao hilo Morrison alishangilia kwa mtindo ambao hupendwa kutumiwa na nyota wa Namungo, Stephen Sey kwa mtindo wa kupunga.


Morrison amesema:”Nilipanga kushangilia kwa mtindo tofauti ila nilikatazwa na wachezaji wenzagu ikiwa ni pamoja na Erasto Nyoni, pia Zraine, (Adel ambaye ni kocha wa viungo) naye alinizuia pia.

“Nilifanya hivyo kwa kuwa nilimwambia awali kwamba lazima tutawafunga nami nilikuwa ninapambana kufunga kwa namna yoyote ilipotokea sikuwa na chaguo zaidi ya kupunga.

“Pia mimi na Sey wote ni marafiki kwa kuwa tunawasiliana na kuongea mambo mengi hivyo hamna tatizo kati yangu na yeye,” amesema.

SOMA NA HII  KUELEKEA DK ZA MWISHO ZA USAJILI KUFUNGWA TZ....SINGIDA BS WAIVURUGA SIMBA KWA ONYANGO...ISHU YOTE NZIMA IKO HIVI...