Home Uncategorized MTANZANIA MWENGINE AIBUKA MSHINDI WA JACKPOT YA SPORTPESA YA MILIONI 437,631,320

MTANZANIA MWENGINE AIBUKA MSHINDI WA JACKPOT YA SPORTPESA YA MILIONI 437,631,320




Mkazi wa jiji la Dar es Salaam Bwana Yassin Ridhiwani Ally ameibuka mshindi katika jackpot SportPesa wiki hii kwa kujishindia kitita cha zaidi ya Tshs milioni 437.


Bwana Yassin mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Ubungo jijini Dar-es-Salaam, amejishindia kiasi cha Tzs 437,631,320 baada ya kubashiri mechi 13 kwa usahihi katika juma linaloishia tarehe 09 Februari 2020.


Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza mshindi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania Bwana Tarimba Abbas alisema kuwa Bwana Yassin ameshinda jackpot hiyo baada ya kubashiri mechi 13 zilizochezwa mwishoni mwa wiki kwa usahihi.


 “Nichukue fursa hii kumtangaza mshindi mpya wa wiki hii wa jackpot yetu ya SportPesa. Bwana Yassin Ridhiwani Ally, Kwa kweli ndoto yake imetimia kama alivyokua akitamani. Naomba kuwahimiza wapenzi wote wa michezo kuendelea kubashiri nasi kwani kila wiki SportPesa inatoa mamilionea.”


Aliongeza na kusema, “kutokana na ushindi wake huu, Bwana Ally atalipa kwa mujibu wa sheria za kodi sawa na asilimia 20% ya zawadi yake, kodi atakayolipa itakuwa ni Tshs. 87,526, 264 ambayo itaenda serikalini moja kwa moja”.


“Niwakumbushe mwaka jana mwezi Agosti tulipata washindi wawili waliopata kila mmoja zaidi ya milioni 414, kisha mwezi mmoja baadae tukapata mshindi wa kwanza wa Jackpot mwanamke aliyeshinda Zaidi ya milioni 260, hivyo tunamkaribisha Bwana Yassin kuwa ni miongoni mwa familia ya washindi”. Alisema Bwana Tarimba.


 “Nachukua fursa hii kuwashukuru kila mdau kwa kutuunga mkono tangu SportPesa ilipofungua ofisi zake hapa Tanzania mwaka 2017. Juhudi za Watanzania ndio zimefanikisha sisi kuendeleza maendeleo ya michezo mbali mbali hapa nchini,” Abbas alisema.


“Nawashauri Watanzania wabashiri na SportPesa kwa kucheza michezo mbali mbali kulingana na vile wanavyopenda. Pia ukishinda malipo ni papo hapo”. Alimaliza Bwana Tarimba.
SOMA NA HII  SIMBA WAPO KWENYE HESABU ZA KUMVUTA NDANI KIUNGO HUYU MATATA