Home Habari za michezo IMEISHA HIYO…’NINJA’ SASA NI MALI YA DODOMA JIJI…ISHU YAKE YAPELEKWA KIMYA KIMYA...

IMEISHA HIYO…’NINJA’ SASA NI MALI YA DODOMA JIJI…ISHU YAKE YAPELEKWA KIMYA KIMYA MPKA KUFIKIA HAPA…


Beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ rasmi sasa yupo tayari kuitumikia Dodoma Jiji kwa mkopo.

Ninja anayemudu kucheza namba tano ama sita hakuwa na nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Kocha Nasreddine Nabi na mara nyingi aliwatumia Bakar Mwamnyeto, Dickson Job ama Yannick Bangala.

Beki huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa nchini Marekani katika klabu ya La Galaxy, Julai mwaka huu aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Yanga kabla ya kutolewa kwa mkopo ili apate nafasi zaidi ya kuendeleza kipaji chake na Dodoma wakambeba.

Tayari beki huyo ameungana na wenzake, lakini benchi linakuna kichwa na kuona anaweza kuwafaa pale nyuma kucheza na Jimmy Shoji, Agustino Nsata, Amani Kyata ama nahodha Mbwana Kibacha.

Dodoma Jiji katika michezo miwili imeruhusu mabao matano dhidi ya Mbeya City 3-1 na Tanzania Prison 2-1.

Akizungumza Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji wa Dodoma Jiji, Dickson Kimaro alisema tayari wamemalizana na mchezaji huyo kwa mkopo.

Kimaro alisema “Ni kweli tumemalizana nae kwa mkopo mshahara wake tutalipa sisi ila kama kulikuwa na madai alikuwa anayadai atamalizana na Yanga sisi tutahusika na mshahara wake.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUONGOZA LIGI..KUHUSU ISHU YA YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU, DIARA KAFUNGUKA HAYA...