Home Habari za michezo WAKATI RAIS SAMIA AKITANGAZA NEEMA KWA YANGA…MBOWE NAYE ATIA NENO…MSIMAMO WAKE HUU...

WAKATI RAIS SAMIA AKITANGAZA NEEMA KWA YANGA…MBOWE NAYE ATIA NENO…MSIMAMO WAKE HUU HAPA..

Habari za Michezo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewapa matumaini wachezaji na viongozi wa Yanga kwa kushindwa kutwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

Yanga juzi usiku ilikuwa Uwanja wa Stade du 5 Juillet kucheza mechi ya pili fainali CAFCC dhidi ya USM Alger na mshindi alipatikana kwa sharia ya mabao ya ugenini na nyumbani ambapo USMA walishinda mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na jana Yanga ilishinda bao 1-0 ambalo halikuweza kuwafanya kuwa mabingwa.

Kupitia mitandao ya kijamii rasmi anayotumia Mbowe ameandika; “Mimi ni muumini wa kutokukata tamaa, ni muumini mzuri pia wa kupambania ninachokiamini kwa gharama yoyote, na ndicho Yanga mlichokionyesha jana,”

“Asanteni kwa hili, pongezi za dhati kwa kuweka alama kwenye mashindano ya kimataifa ya CAFCC, sina shaka wakati ujao tutalibeba kabisa kombe. Pongezi za dhati kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi wa klabu na mashabiki kwa kujitoa kwenu kwa hali na mali. Mmeliheshimisha Taifa,”

Aidha katika upande mwingine, Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa kile walichokifanya nchini Algeria na kwamba wanatakiwa kurudi nyumbani vifua mbele.

“Vijana wa @yangasc msilie, taifa letu mmelifanyia jambo kubwa sana, nyie hamjui tu. Rudini nyumbani mkiwa vifua mbele!”

Juni 3,2023 Yanga iliandika historia ya kushinda ugenini 1-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo wa marudiano ya Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, ,lakini ikalikosa taji kutokana na faida ya bao la ugenini na kuwabeba USM Alger.

SOMA NA HII  DILI LA KIBU DENIS LAJIBU, KUIBUKIA JANGWANI KWA DAU LA MILIONI 150

1 COMMENT