Home Habari za michezo KUELEKEA MSIMU UJAO…MO DEWJI KUZIBOMOA AZAM, SINGIDA NA VIPERS…MASTAA HAWA KUTUA SIMBA…..

KUELEKEA MSIMU UJAO…MO DEWJI KUZIBOMOA AZAM, SINGIDA NA VIPERS…MASTAA HAWA KUTUA SIMBA…..

Habari za Simba SC

Sahau kuhusu matokeo ya mechi ya juzi, Simba ilipovaana na Ruvu Shooting. Kwa sasa Wekundu wa Msimbazi wanapiga hesabu za msimu ujao na tayari kocha Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameshawasilisha ripoti yake kwa mabosi wa klabu hiyo akitaka kushusha kikosi kizima.

Ndio, Ropbertinho amepanga kusajili wachezaji 11 kwa nafasi tofauti kuanzia ile ya kipa hadi ushambuliaji, kisha kupitisha panga la kufyeka baadhi ya nyota waliopo katika kikosi cha sasa ili mambo yasiwe mengi msimu ujao baada ya msimu huu timu hiyo kutoka patupu kwa msimu wa pili.

Hakuna ubishi, tayari Wanamsimbazi wamekubali yaishe kwa msimu huu kwani kwa mechi zilizobaki wanacheza tu ili kukamilisha ratiba, huku ikiwa imeshang’olewa kwenye michuano ya Kombe la ASFC na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa sasa kuanzia kwa uongozi, benchi la ufundi na wachezaji kila mmoja anauwaza msimu ajao ambao wamepanga kufanya mapinduzi makubwa ili mnyama arudi kwenye Ligi Kuu Bara na michuano mingine ikiwamo ya kimataifa ikiwa na nguvu na kurejesha heshima.

Wakati vikao vya mara kwa mara vikiendelea ndani ya ofisi za Simba na kambini, Mwanaspoti limepenyezewa tayari timu hiyo imeanza usajili kimyakimya na hadi sasa imenasa saini ya beki mmoja na iko njiani kukamilisha dili zingine, ikiwamo kwa kiungo mkabaji kutoka Azam na kipa anayejua kudaka wa Vipers ya Uganda.

Katika orodha hiyo ya wachezaji hao 11 ambao Mbrazili amependekeza kwa kila eneo ni kuletwa viungo wakabaji wapya wawili, viungo washambuliaji wawili, beki wa kushoto mmoja, beki wa kati wawili, kipa mmoja, winga asilia wawili na mshambuliaji mmoja.

Ujio wa wachezaji hao utaenda kuziba mapengo ya Beno Kakolanya aliyesajiliwa na Singida Big Stars, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Ismail Sawadogo, Agustine Okrah, Peter Banda, Jimmyson Mwanuke, waliopo kwenye mpango wa kuachwa pamoja na Moses Phiri na Joash Onyango walioomba kuondoka kikosini hapo.

Mwanaspoti linajua Simba tayari imemsajili beki wa kushoto Yahya Mbegu kutoka Ihefu atakayeziba pengo la Gadiel, ili kuungana na nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ katika eneo hilo lakini ipo kwenye mazungumzo mazuri na wachezaji wengine kutoka ndani na nje ya nchi.

Viungo Sospeter Bajana, anayemaliza mkataba wake na Azam msimu huu sambamba na Mbrazil wa Singida United Bruno Gomez ambaye kocha Robertinho amewaambia mabosi wa Msimbazi wamlete kwa gharama zozote ni miongoni mwa wachezaji wanaoendelea na mazungumzo na Simba.

Wengine walio kwenye rada za Simba ni kipa Mrundi Fabien Mutombola na mshambuliaji Mganda Martin Kizza wote kutoka Vipers waliofundisha na kocha Robertinho kabla ya kutua Msimbazi.

Simba inataka kukamilisha usajili wote mapema ili iwezekanavyo ili wachezaji wote waingie kambini kwa pamoja baada ya mapumziko ya kumalizika kwa msimu na kulipa bechi la ufundi muda wa kutosha kusuka kikosi kipya.

Pia huenda benchi la ufundi likawa na mabadiliko kwani ambapo Juma Mgunda anaweza kuondoka kikosini hapo kutokana na maelewano hafifu na Robertinho lakini pia kocha wa viungo, ‘Msauzi’ Kelvin Mandla yupo kwenye mpango wa kufungashiwa virago huku Adel Zrane aliyewahi kufanya kazi hiyo Msimbazi akitajwa kurejea.

Nguvu yote hayo ni kutokana na kukosa taji lolote msimu huu, sambamba na Simba kucheza soka la kawaida tofauti na ilivyozoeleka.

SOMA NA HII  MPANGO WA SIMBA KUWASHUSHA AL AHLY BONGO UKO NAMNA HII...MANGUNGU AFUNGUKA A-Z

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here