Home Habari za michezo ALIYEWAHI KUKIPIGA KLABU ZA ULAYA AWAITA SIMBA MEZANI…JAMAA NI ‘MKATA SHOMBO’ HASWA..

ALIYEWAHI KUKIPIGA KLABU ZA ULAYA AWAITA SIMBA MEZANI…JAMAA NI ‘MKATA SHOMBO’ HASWA..

Tetesi za usajili Simba

Kiungo Mkabaji kutoka nchini Ethiopia na Klabu ya Saint George Gatoch Panom Yiech amesema yupo tayari kusajiliwa Simba SC, endapo atapata ofa nzuri itakayong’oa nchini kwao.

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa huenda wakasajiliwa Simba SC, iliyodhamiria kuboresha kikosi chake kwa msimu ujao, baada ya kutoka kapa msimu huu 2022/23.

Yiech ambaye anamudu kucheza nafasi za kiungo amewahi kucheza soka la kulipwa Anzhi Makhachkala ya Urusi, Haras El Hodoud ya Misri, Al-Anwar ya Saudi Arabia na nyinginezo, amesema anaifahamu Simba SC na aliwahi kucheza nayo kwenye Simba Day akiwa na St George.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, ameendelea kusema kuwa, mpaka sasa hajapokea ofa rasmi kutoka Simba SC lakini kama watampa mkataba mnono yuko tayari kujiunga nao kwa kuwa soka ni kazi yake.

Amesisitiza kuwa amekuwa akivutiwa na klabu hiyo namna ambayo imekuwa ikipambana hususan katika Michuano ya kimataifa na hata Ligi ya ndani.

“Naifahamu Simba SC kwa kuwa niliwahi kucheza dhidi yao kwenye Simba Day mimi nikiwa na timu yangu ya St George. Ni timu nzuri na ninaipenda.”

“Kuhusu kujiunga nao mpaka sasa hawajaleta ofa rasmi. Hata wakileta itategemea na ofa yao itakavyokuwa lakini ni timu nzuri na niko tayari kuja kufanya nao kazi,” amesema kiungo huyo mwenye mwili mkubwa

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO....MINZIRO APAZA SAUTI KWA UONGOZI WA GEITA...AFUNGUKA YOTE KUHUSU USAJILI WA MASTAA WAPYA....