Home kimataifa LUKAKU BADO YUPO INTER

LUKAKU BADO YUPO INTER


 MSHAMBULIAJI  wa kikosi cha Inter Milan, Romelu Lukaku amesema kuwa atabaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa anafurahi maisha ya hapo licha ya kuhusishwa kusepa ndani ya Serie A.

Nyota huyo ambaye alijiunga na Inter Milan akitokea Manchester United amekuwa akitajwa kurudi ndani ya Ligi Kuu England msimu ujao jambo ambalo ameligomea.

Msimu uliopita kwenye Serie A alitupia jumla ya mabao 24 na kuipa ubingwa timu yake baada ya miaka 11 jambo ambalo limefanya thamani yake izidi kuwa kubwa na kuzivutia timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England ambapo Chelsea ilikuwa inatajwa kuivutia saini yake.

Lukaku ambaye ni raia wa Ubelgiji amesema kuwa anajisikia furaha ndani ya Inter Milan jambo ambalo litamfanya abaki katika kikosi hicho msimu ujao hivyo mashabiki wasiwe na mashaka juu yake.

“Nipo na nitabaki ndani ya Inter Milan kwani hapa ni sehemu nzuri kwangu na maisha yake ninayafurahia,”.

SOMA NA HII  HAALAD FITI KUANZA KAZI LEO MBELE YA SEVILLA