Home EURO 2020 URENO YAWAAMBIA MASHABIKI WAKAE MKAO WA KULA

URENO YAWAAMBIA MASHABIKI WAKAE MKAO WA KULA


 JOAO Moutinho amewaambia mashabiki wa timu ya taifa ya Ureno kuwa wakae mkao wa kula kwa kuwa watarudisha furaha kwao.

Ureno walinyooshwa mabao 4-2 dhidi ya Ujerumani kweye mchezo wa Euro 2020 juzi jambo ambalo lilizua hofu kuhusu suala la kuweza kufuzu michuano hiyo hatua ya mtoano.

Nyota huyo amesema kuwa mchezo wao leo dhidi ya Ufaransa utakuwa mkali na mashabiki wakae tayari kuona kile ambacho watakifanya.

“Tunajua jinsi ambavyo mashabiki waliumia, nafikiri mwisho wa uchungu umefika na sasa wasubiri matokeo mazuri,” .

Ureno ni mabingwa watetezi wana pointi tatu baada ya kushinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja, leo saa 4:00 usiku wana kazi ya kufanya mbele ya Ufaransa. 

SOMA NA HII  VIDEO: MASHINDANO YA EURO YAWAPAGAWISHA MASHABIKI