Home Yanga SC YANGA YAPIGA HESABU YA POINTI 15 BONGO

YANGA YAPIGA HESABU YA POINTI 15 BONGO


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba mechi zao tano ambazo zimebaki sawa na dakika 450 watapambana kushinda ili kupata pointi tatu zitakazowapa jumla ya pointi 15.


Mechi zao ambazo zimebaki kwa sasa baada ya kucheza mechi 29 ni Juni 17  dhidi ya Ruvu Shooting, Juni 20 ni dhidi ya Mwadui, Julai 3 dhidi ya Simba, Julai 14 dhidi ya Ihefu na kigongo chao cha mwisho ni Julai 18 dhidi ya Dodoma Jiji.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wanahitaji pointi tatu katika kila mechi kwa kuwa wanajua umuhimu wa pointi hizo na nia yao ni kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

“Hatujakata tamaa kuhusu ubingwa kwani tuna mechi tano mkononi, katika hizo mechi tano tumepanga kushinda zote kisha baada ya ligi kukamilika hapo tutajua kwamba tumevuna nini na tunastahili kupata nini.

“Hao wanaoongoza ligi ikumbukwe kwamba wana viporo, sasa wakimaliza kucheza hizo mechi kisha tukiwa nao tumecheza mechi sawa itafahamika tu mwisho wa ligi,” alisema Bumbuli.

Vinara wa ligi ni Simba wana pointi 67 baada ya kucheza mechi 27 na Yanga wamecheza mechi 29 wana pointi 61.

SOMA NA HII  BAADA YA KUUWASHA AFCON...AZIZ KI KUPIGWA BEI YANGA?....UKWELI WOTE HUU HAPA...