Home kimataifa SUALA LA MUDA TU KUTAMBULISHWA MANCHESTER UNITED CR 7

SUALA LA MUDA TU KUTAMBULISHWA MANCHESTER UNITED CR 7


MANCHESTER United wamekubali kumrejesha nyota wao wa zamani Cristiano Ronaldo mwenye miaka 36 ndani ya Old Trafford akitokea Juventus huku wakipindua meza mapema mbele ya Manchester City ambao wao walikuwa tayari kumpa dili la miaka miwili pia.

Tayari Ronaldo raia wa Ureno ambaye alifunga jumla ya mabao 118 ndani ya Manchester United kati ya msimu wa 2003 mpaka 2009 aliyeweza kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu England pamoja na lile taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ameshawaaga mashabiki na mabosi wake wa Juventus ni suala la muda kutambulishwa ndani ya United.

Jana na leo kwenye mitandao ya kijamii kuanzia kwenye tweeter mpaka Instagram ilikuwa ni habari ya usajili wa Ronaldo kwa kuwa alikuwa anapewa nafasi kubwa kuibukia Uwanja wa Etihad ila mambo yakabuma ghafla na United wakaingilia kati na kuhitaji kusepa na saini ya mchezaji wao wa zamani.

Imeyeyuka miaka 12 baada ya nyota huyo kusepa ndani ya Manchester United na alipokuwa ndani ya Real Madrid na Juventus  aliweza kufunga jumla ya mabao 551 katika mechi 572 huku mshikaji wake Bruno Fernandez akijiita wakala wa mchezaji huyo kwa kuwa anadai alimshawishi aweze kurejea United.

SOMA NA HII  KANE AWAOMBA MABOSI WAPOKEE OFA