Home kimataifa JESSE ACHEKELEA KUFUNGA TIMU YA TAIFA

JESSE ACHEKELEA KUFUNGA TIMU YA TAIFA


JESSE Lingard nyota wa timu ya taifa ya England amesema kuwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja kwenye timu yake ya taifa ni moja ya jambo linalompa furaha na anaamini itaendelea kuwa hivyo.

Nyota huyo ametupia katika timu yake ya taifa zikiwa zimeyeyuka jumla ya siku 1,022 kwa kuwa mara ya mwisho Lingard kufunga bao kwa timu yake ya taifa ilikuwa ni Novemba 2018 walipocheza dhidi ya Croatia, Uwanja wa Wembley. 

Lingard alipachika mabao mawili mbele ya timu ya taifa ya Andorra na England ilishinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia na timu hizo zipo kundi I.

Baada ya kufunga na kutoa pasi nyota huyo alikuwa na furaha na alishangilia kwa mtindo wa Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa ni mali ya Manchester United.

Mabao ya Lingard ilikuwa dakika ya 18 na 78 mengine yalifungwa na Harry Kane ambaye ni nahodha kwa penalti dk ya 72 na Bukayo Saka dk 85.


SOMA NA HII  MWAKINYO 'AJIBU SHOMBO' ISHU YA KUVULIWA UBINGWA AFRIKA...ADAI HAUNA THAMANI KIIIVYOOO...