Home Yanga SC YANGA YAWAITA WANACHAMA KWA WINGI KUWA SEHEMU YA HISTORIA

YANGA YAWAITA WANACHAMA KWA WINGI KUWA SEHEMU YA HISTORIA


LEO Juni 27 Klabu ya Yanga imepanga kufanya mkutano mkuu wa kawaida wenye ajenda 12 zilizoanishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Mshindo Msola kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.

Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa DYCCC, Chang’ombe, Dar kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.

Wanaoruhusiwa kuwasili katika mkutano huo ni wanachama hao wa Yanga ambao wameshalipia kadi zao na zoezi hilo la ulipaji ni endelevu kwa Wanachama wa Yanga.

Kwa mujibu Msolla amesema kuwa moja ya ajenda muhimu n pamoja na wanachama kupitisha mfumo mpya wa uendeshaji ndani ya Klabu ya Yanga.

Msolla amesema:-“Wanachama kupitisha mfumo mpya wa klabu yetu, hili ni jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisubiriwa yamekuwa ni matamanio ya Wanayanga wengi, sasa hatimaye uongozi wenu umeweza kufanikisha jambo hilo.

“Niwaombe wanachama ambao watakuja kwenye mkutano wajichukulie kwamba wao ni sehemu ya historia ya kubadili muundo wa klabu yetu, tuna imani kubadili muundo itafanya timu iendeshwe kisasa,” .

SOMA NA HII  HIYO VITA YA NAMBA YANGA ACHA KABISA