PRINCE Dube nyota wa kikosi cha Azam FC kuna hatihati ya KUIKOSA tuzo ya mfungaji bora kutokana na kusumbuliwa na tatizo la tumbo.
Nyota huyo raia wa Zimbabwe ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Azam FC akiwa ametupia mabao 14 sawa na John Bocco wa Simba ambaye anapewa nafasi ya kuipoka tuzo hiyo.
Mtetezi wa tuzo hiyo ni Meddie Kagere mwenye mabao 11 naye bado anapewa nafasi ya kuweza kusepa na tuzo hiyo kwa kuwa bado Simba ina mechi mkononi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa nyota huyo amefanyiwa vipimo mara tatu ila katika hali ya kushangaza tatizo limekuwa likijirudia.