Yanga SC

JEMBE JIPYA LA YANGA LABAKIZA DAKIKA 180 KUIBUKA KIKOSINI

admin July 8, 2021 1:47 pm


JEMBE jipya ambalo kwa asilimia 50 limekamilisha masuala yote kuhusu kujiunga na Yanga, Dickson Ambundo amebakisha dk 180 kujiunga na mabosi wake hao wapya.


Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa kiungo huyo mshambuliaji imeeleza kuwa tayari makubaliano ya nyota huyo na mabosi wa Yanga yamefika sehemu nzuri hivyo anachosubiri kwa sasa ni kumaliza mkataba wake ili aibuke Yanga.

“Uwezekano ni mkubwa kwa Ambundo kujiunga na Yanga msimu ujao kwa sasa anasubiri kumaliza mechi zake mbili ambazo zimebaki ndani ya Dodoma Jiji kisha ataanza maisha yake mapya Yanga,” ilieleza taarifa hiyo.

Mechi mbili ambazo Dodoma Jiji imebakiwa nazo ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Julai 14 na ule dhidi ya Yanga, Julai 18 ambazo ni sawa na dk 180.

Ambundo amesema kuwa kwa sasa bado anaendelea kazi yake ndani ya Dodoma Jiji hivyo itajulikana msimu utakapoisha.

”Tusubiri na tuone itakuaje kwani bado nipo Dodoma Jiji kwa sasa,” .

Ikiwa Dodoma Jiji ipo nafasi ya 9 imekusanya jumla ya pointi 42 baada ya kucheza jumla ya mechi 32.

SAMATTA – YANGA WAMSHUKURU MORRISON VIDEO: MSHAMBULIAJI WA ZAMBIA, MOSES PHIRI ANAKUJA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply