news

ISHU YA SIMBA V YANGA KUPIGWA KWA MKAPA IPO HIVI

admin July 15, 2021 1:47 pm


CLIFFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema kuwa fainali ya Kombe la Shirikisho itapigwa kulekule Kigoma.

Imekuwa ikielezwa kuwa kuna mpango wa mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Julai 25 unaweza kuletwa Uwanja wa Mkapa.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba huenda mchezo huo ukachezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na fainali hiyo kuwakutanisha Yanga v Simba.

Ndimbo amesema:”Hizo ni tetesi tu za kubadilisha uwanja, mchezo utapigwa hapohapo Uwanja wa Lake Tangayika, Kigoma,”.

Ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo watapambana na watani zao wa jadi Yanga. 

HARUNA NIYONZIMA KUAGWA LEO KWA MKAPA KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA IHEFU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply