Yanga SC

MAKAMBO AAGWA RASMI HOROYA, DILI LAKE KUTUA YANGA LAWA JEPESI

admin July 19, 2021 5:47 pm


 KLABU ya Horoya leo Julai 18 iketangaza rasmi kusitisha mkataba na mchezaji wao Heritier Makambo.

Kupitia katika ukurasa rasmi wa Horoya ya Guinea wameandika kwamba wanashukuru kwa huduma ya mchezaji huyo ambaye amedumu hapo kwa muda wa misimu miwili.

Nyota huyo aliibuka hapo akitokea Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mfungaji namba moja Yanga alipotupia mabao 17 na kuwa namba tatu kwa washambuliaji wenye mabao mengi.

Huenda dili lake la kurudi Yanga likajibu kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi hao ambao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.

Hivyo kuangwa kwake rasmi na mabosi wake hao kunafanya dili lake kuwa jepesi kuweza kutua Yanga.

MOHAMED HUSSEIN ACHEKELEA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU BARA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply