Home Simba SC GOMES ALIANZISHA MSIMBAZI..AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE KWA MSIMU UJAO

GOMES ALIANZISHA MSIMBAZI..AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE KWA MSIMU UJAO


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema anawaza kufanya vizuri zaidi kimataifa baada ya klabu hiyo kutengeneza rekodi kubwa katika mashindano ya ndani.

Gomes alisema katika mashindano ya ndani wamechukua Kombe la Ligi na Azam kwa mara pili mfululizo na sasa wanataka kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kimataifa.

“Tunataka kuwa vizuri zaidi msimu ujao hasa kwenye mashindano ya kimataifa, tulipoishia msimu huu tunataka tufike mbali zaidi katika msimu ujao na naamini tutafanya hivyo,” alisema.

Katika kuhakikisha hilo, Gomes amewapa mapumziko ya siku 10 wachezaji kuanzia jana Jumatatu na baada ya hapo watarejea kambini kwa ajili ya maandalizi msimu ujao.

“Hatuna muda mrefu wa kujiandaa, kama unavyojua Septemba inaanza Ligi ya Mabingwa tunatakiwa tuanze mazoezi ya nguvu mapema ili wachezaji waweze kuwa fiti.”

Akizungumzia upande wa kuchukua makombe yote mawili ya ndani, Gomes alisema hiyo inaonyesha ubora wa kikosi chake ndani ya Tanzania.

“Ni wazi kwamba Simba ni timu kubwa hapa Tanzania na hii ni zawadi kubwa kwa mashabiki wetu kwa kuwapa vikombe viwili kwa msimu huu na tumekuwa bora,” alisema.

“Msimu ujao tutazidi kuwa bora zaidi ya hapa na kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wamekuwa nasi kwa siku zote.”

KAMBI MISRI

Simba baada ya kumaliza mapumziko ya siku 10 itarejea kambini na kuondoka kwenda nchini Misri Agosti 8 kuweka kambi mpaka Agosti 28.

Wakiwa nchini humo mabingwa hao wa Bara watacheza mechi za kirafiki kwa ajili ya utimamu wa miili ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu

SOMA NA HII  FT: SIMBA 3-0 GEITA GOLD.... OKRAH, PHIRI NA CHAMA WAFANYA YAO....'MZUNGUU' BADO SANA..AINGIA NA ZALI...