Home Azam FC KIUNGO MKABAJI, INGIZO JIPYA LA AZAM: NATAKIWA KUFANYA KAZI

KIUNGO MKABAJI, INGIZO JIPYA LA AZAM: NATAKIWA KUFANYA KAZI

 PAUL Katema, ingizo jipya ndani ya Klabu ya Azam FC akitokea Klabu ya Red Arrows amesema kuwa anatakiwa kufanya kazi ili kuongeza mchango wake katika timu hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Nyota huyo raia wa Zambia ambaye ni kiungo mkabaji ametangazwa ndani ya Azam FC kwa kusaini dili la miaka miwili akiwa ni kiungo hivyo anaongeza nguvu zaidi eneo hilo kwa ajili ya msimu ujao.

Anakuwa ni nyota watano kutambulishwa rasmi Azam FC baada ya Charlse Zulu,  Rodgers Kola, Kenneth Muguna na Edward Manyama kutambulishwa. 

Nyota huyo amesema:”Awali ya yote ningependa kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi hii ya mimi kuwa hapa. Najisikia vizuri.Nadhani natakiwa kufanya kazi. Nimekuja hapa kuifanyia kazi timu hii. Kuongeza kiłe nilichonacho kwa aijli ya kutoa mchango kwa timu.

“ili timu isonge mbele. Vinginevyo, najisikia vizuri sana kusaini kuitumikia Azam. Niliwahi kusikia habari za Azam, na baadaye nikaja hapa na timu yangu Red Arrows, tukacheza mechi ya kirafiki. Nilivutiwa sana na uwanja wao, nilivutiwa na miundombinu ambayo wanayo, nilishaisikia kabla.”

SOMA NA HII  PRINCE DUBE APEWA PROGRAM MAALUMU KURUDI KWENYE UIMARA