Home Uncategorized MNATA ATAJA ANACHOKIPATA KUTOKA KWA SHIKALO

MNATA ATAJA ANACHOKIPATA KUTOKA KWA SHIKALO


METACHA Mnata, mlinda mlango namba mbili wa Yanga amesema kuwa anakubali uwezo wa mlinda mlango namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo kutokana na kuwa na vitu tofauti.

Shikalo raia wa Kenya ni mlinda mlango namba moja huku namba mbili akiwa ni Mnata ambaye ni mzawa.

Mnata amesema:”Nimekuwa nikijifunza mengi kupitia kwa Shikalo ambaye ni kipa mwenzangu ndani ya Yanga, jambo hilo linanifanya nami nizidi kujifunza bila kuchoka.

“Ukiwa mlinda mlango una kazi kubwa ya kuokoa na kujifunza pale ambapo unakuwa upo benchi hivyo wakati ule ligi ilipokuwa inaendelea nilikuwa ninajifunza mengi,”.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimesababisha ligi nyingi duniani kusimamishwa.


SOMA NA HII  CCM KIRUMBA TENA KUWAKA MOTO LEO, ALLIANCE V SIMBA VITA YA KISASI