Home KMC FC KMC WAFUNGUKIA ISHU YA KUMKODI MZEE MPILI

KMC WAFUNGUKIA ISHU YA KUMKODI MZEE MPILI

WAKATI leo Julai 7 Klabu ya KMC ikitarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Simba, mabosi wa timu hiyo wamefungukia ishu ya kudaiwa kumkodi Haji Omari Mpili, maarufu kama Mzee Mpili.
Jana, Julai 6 ilisambaa twiter iliyokuwa inaonesha kwamba inamilikiwa na Klabu ya KCM ambayo ilisomekana namna hii:”Tumemkodi kwa muda Mzee Mpili, mtajua amjui,”.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa akaunti hiyo sio yao na wala hawana mpango wa kufanya hivyo.
“Hiyo akaunti siyo yetu na hatuijuia kabisa kwa kweli, hatuna mpango wa kufanya hivyo vijana wetu wapo vizuri na maandalizi yapo sawa,” .
Mzee Mpili amekuwa akitamba kwamba ushindi wa Yanga walioupata Julai 3 wa bao 1-0 dhidi ya Simba ni yeye alikuwa mchezaji namba moja jambo ambalo lilifanya KMC wadai kwamba nao watamkodi kwa muda.
Mpili alisikika akisema kuwa:”Ushindi wa Yanga mimi nilikuwa mchezaji namba moja hivyo hakukuwa na namna kwa Simba kutufunga ilikuwa lazima wafungwe kwa kuwa mimi nina watu,” .

 

SOMA NA HII  KMC WANAHESABU NDEFU MSIMU MPYA 2021/22