Home news KUMBE! PILATO WA MECHI YA SIMBA V YANGA, FAIDA KWA SIMBA

KUMBE! PILATO WA MECHI YA SIMBA V YANGA, FAIDA KWA SIMBA



MWAMUZI wa mtanange wa Yanga dhidi ya Simba kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Shirikisho la Azam (ASFC), Ahmed Arajiga, amechezesha michezo miwili ya Simba ambayo yote wameshinda na kufikia hatua ya fainali.

Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani leo Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma ukiwa ni mchezo wa kumtafuta bingwa wa michuano ya ASFC.

Takwimu zinaonyesha kuwa mwamuzi, Arajiga ni faida kwa Simba ambapo kwenye michezo miwili ya ASFC aliyochezesha ambayo ni ya Robo fainali na Nusu fainali, Simba wameshinda.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa Mei 26, mwaka huu.

Mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Azam FC, uliopigwa Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mwamuzi huyo mwenyeji wa mkoani Manyara hajachezesha mchezo wowote wa Yanga kwenye michuano ya Shirikisho la Azam kwa msimu huu. 

Kuhusu suala la mwamuzi huyo, Yanga waliandika maoni kwamba uteuzi wa mwamuzi huyo wanaona kama hawajauelewa kwa kuwa amechezesha mechi nyingi za wapinzani wao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania, Sud Abdi alitoa taarifa kwamba sababu mojawapo inayofanya waweze kumteua mwamuzi ni pamoja na mechi ambazo amechezesha uwezo wake pamoja na vigezo vingine ambavyo wanazingatia.

Hata Ulaya amebainisha kuwa huwa wanafanya hivyo kwa kumchukua mwamuzi kulingana na mashindano amechezesha katika mashindano husika.


SOMA NA HII  KUHUSU MVUA YA MATAJI YANGA MSIMU UJAO...SENZO AENDELEA 'KUWABAGAZA' SIMBA KWA MANENO...